Kwa uchache watu 13 waliuawa katika shambulio dhidi ya gari katika mji wa Donetsk, Alhamisi Januari 22 mwaka 2015.
Na RFI
Watu
thelathini na wanne wameuawa ndani ya masaa 24 Mashariki mwa Ukraine.
Hata hivyo wito wa kusitisha mapigano uliyotolewa Jumatano Januari 21
mjini Berlin na Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani, Urusi,
na Ukraine umepuuzwa.
Shambulio
baya lililosababisha maafa makubwa limetokea Alhamisi Januari 22
asubuhi katika mji wa Donetsk, Mashariki mwa Ukraine. Shambulio hilo
limegharimu maisha ya watu 13, baada ya gari waliokuwemo kushambulio kwa
bomu.(P.T)
Shambulio
limetokea katika kata ya Kusini Magharibi mwa Donetsk, kata ambayo
ilikua bado haijaguswa na mapigano. Gari waliyokuwemo watu hao
limeteketea.
Waangalizi
wa jumuiya inayohusika na usalama na ushirikiano barani Ulaya wamefika
eneo la tukio ili kujaribu kujua sababu za shambulio hilo.
Jeshi la Ukraine na waasi mara mara, wamekua wakitupiana lawama na kunyoosheana kidole kuhusika na shambulio hilo.
Ikijaribu
kujitetea, Wizara ya ulinzi ya Ukraine imethibitisha kwamba eneo
kulikotokea shambulio ni kwenye umbali wa kilomita 15 na eneo
kunakopatikana askari wa Ukraine.
Jeshi
limepata pigo kubwa kwa mashambulizi hayo yanaoendelea Mashariki mwa
Ukraine. Wanajeshi kumi wa Ukraine waliuawa saa 24 zilizopita, huku
askari wakiondoka katika uwanja wa Donetsk, na kwa sasa uwanja huo
unadhibitiwa na waasi.
Waziri
mkuu wa Ukraine ameishtumu Urusi kuhusika katika shambulio dhidi ya gari
hilo liliyotokea leo Alhamisi na kusababisha vifo vya watu 13. Kwa
upande wake, Urusi umelinyooshea jeshi la Ukraine kuhusika na shambulio
hilo.
No comments:
Post a Comment