Abiria wahofia usalama wa Kivuko cha Mv. Magogoni
23rd January 2015

Kivuko cha Mv. Magogoni
Hatua hiyo imefuatia matukio ya kuharibika mara kwa mara nyakati za
usiku na kuchukua muda majini huku kikiwa na abiria na magari.
Fadhili Mbaga, mkazi wa Kigamboni, alisema, Serikali inapaswa
kuangalia kwa makini suala la usalama wa abiria wa Feri ambao wanatumia
usafiri huo, kutokana na kivuko hicho kutokuwa na sifa za kusafirisha
abiria wengi na mizigo kwa wakati.
“Abiria tumekuwa na wasiwasi na huu usafiri kwani mara nyingi
injini ya kivuko hiki siyo nzima na kusababisha ofu kubwa kwetu,”
alisema.
Anna Mwasombe, mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere, alisema kutokana na ubovu wa kivuko hicho, abiria wengi
wasiokuwa na haraka hulazimika kusubiri kupanda kivuko cha MV Kigamboni.
“Mara nyingi kivuko hiki kikiwa kinafanya safari zake hutumia saa
nyingi kufika upande wa pili kutoka na kuelemewa, hivyo kusababisha
abiria kutumia muda mrefu kufika kutokana na kutembea taratibu,”
alisema.
Samson Gama, alisema Serikali kwa kushirikiana na Wakala wa Ufindi
na Umeme (Temesa) inapaswa kufanya ugaguzi kila wakati ili kuhakikisha
vivuko vyote vinakuwa katika hali nzuri na salama kusafirisha abiria.
No comments:
Post a Comment