
Serikali inasema kwamba walinzi wa maduka binafsi ndio waliowaua waandamanaji
Serikali
ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekanusha madai ya kuwauwa
waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga mapendekezo ya kubadilisha
sheria za uchaguzi mkuu.
Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu arubaini wameuawa katika siku tatu za ghasia.BBC
Waziri wa mawasiliano Lambert Mende, aliambia BBC kwamba polisi hawakutumia silaha zozote dhidi ya waandamanaji hao.
Alisema waandamanaji ambao aoliwataja kama waporaji, waliuawa na walinzi waliokuwa wanalinda majengo ya biashara yaliyoporwa
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kwamba zaidi ya watu 40 wameuawa katika siku tatu za vurugu mjini Kinshasa.
Mabadiliko
yaliyopendekezwa huenda yakachelewesha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika
mwaka ujao, wakati Kabila anatarajiwa kung'atuka baada ya kuitawala
nchini huo kwa miaka 14.
No comments:
Post a Comment