
Mwenyekiti
wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma ametangaza mjini
Addis Ababa, Ethiopia kuundwa kwa kikosi cha kimataifa kwa kuanzisha
vita dhidi ya Boko Haram.
Na RFI
Uamzi wa
pamoja umechukuliwa na Umoja wa Afrika wakati wa kikao chake cha Baraza
la amani na usalama Alhamisi Januari 29 jioni mjini Addis Ababa,
Ethiopia na kuhudhuriwa na zaidi ya marais kumi na tano.
Rais wa
Nigeria Goodluck Jonathan na rais wa Cameroon Paul Biya hawakushiriki
kikao hicho. Umoja wa Afrika unaunga mkono kikosi cha kimataifa cha
wanajeshi 7500.(P.T)
Lengo la Umoja wa Afrika ni kushawishi Umoja wa Mataifa kufadhili mashambulizi ya kikosi hicho cha Umoja wa Afrika.
Uamzi huo
umechukuliwa na marais na viongozi wa serikali za Afrika Alhamisi 29
Januari mjini Addis Ababa, ambao wanakabiliwa na tishio la Boko Haram.
Mwezi
ujao, Umoja wa Afrika utakutana rasmi na Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa, ili kuliomba kusaidia, kupitia mfuko wa amani, msaada wa vifaa
na fedha kwa kikosi cha kimataifa chenye wanajeshi 7500, ambao
watatakiwa, kwa mujibu wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Nkosazana
Dlamini-Zuma, kupambana dhidi ya Boko Haram.
Umoja wa
Afrika unaunga mkono jitihada za jumuiya ya nchi zinazochangia Ziwa
Chad, za kuundwa kwa kikosi cha kimataifa kutoka Nigeria, Chad, Cameroo,
Niger na Benin.
Uamzi huu
umechukuliwa na zaidi ya marais kumi na tano ambao ni wajumbe wa Baraza
la amani na usalama, uamuzi ambao unatazamiwa kupitishwa katika mkutano
mkuu wa marais na viongozi wa serikali ambao utadumu siku mbili kuanzia
Ijuma wiki hii.
Nigeria
na majirani zake wameafikiana juu ya msimamo wa pamoja, baada ya miezi
ya kutoaminiana na kutokuelewana. Lakini kama Umoja wa Afrika, kupitia
jumuiya ya nchi zinazochangia ziwa Chad, una wanajeshi, bao unakabiliwa
na ukosefu wa vifaa vya kijeshi na fedha.
No comments:
Post a Comment