
Klabu ya
Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la
kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya
manyanyaso anayoyapata.
Akizungumza
mchana huu katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Habari
Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha malalamiko yao
hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa Tambwe wikiendi
iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo wanataka
mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro
amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua kali
wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka shirikisho
hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa mchezo huo lengo
likiwa ni kujua umakini wa waamuzi hao.(P.T)

“Tatu
tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia kuwachukulia
hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa kubaini haya
ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana wafungiwe na
Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo tutagoma na
hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi wao
kushabikia maovu haya.
Aidha
Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema ameshangazwa kuona
anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi kuyaweka hadharani.
“Mpira ni
starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani unanikaba
hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu wanajua
maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo kiungwana
siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema Tambwe
No comments:
Post a Comment