TAARIFA MTANDAO WA FACEBOOK KUPOTEA DUNIANI KWA DAKIKA 40

Mtandao wa kijamii wa facebook ulikuwa hauingiliki katika maeneo mengi duniani mapema leo kabla ya huduma zake kurudi.
Mamilioni ya watumizi wa mtandao wa facebook walishindwa kuingia katika akaunti zao.
Wateja wake katika mataifa mengine walishindwa hata kutumia hudumu ya Instagram.
Facebook ilisema kuwa
wahandisi wake ndio walioababisha tatizo hilo, na kukana madai kwamba
kundi moja linalotekeleza uhalifu wa mitandaoni lilihusika.
''Awali watu wengi
walikuwa hawawezi kuingia katika akaunti zao za mitandao ya facebook
pamoja na huduma ya Instagram'', msemaji wa facebook aliiambia BBC.
''Hili halikuwa
shambulizi kutoka kwa watu wengine lakini lilitokea baada ya kufanya
mabadiliko ambayo yaliathiri mpangilio wa mfumo wetu''.
Tuliharakisha na kutatua tatizo hilo na sasa huduma zote zimerejelea asilimia 100 kama kawaida
Mitandao hiyo ilitoweka kwa takriban dakika 40 kabla ya kurudi.
Programu ya mtandao
unaowaunganisha wapendanao Tinder ambayo hutegemea facebook ili kutoa
huduma zake pia iliathiriwa na tataizo hilo.
Kundi moja la uhalifu wa
mitandano kwa jina Lizard Squad liliandika ujumbe kwa twitter kuhusu
hudumu hiyo kutoweka na kusababisha ripoti kwamba huenda lilihusika.
Kundi hilo limeshtumiwa
kwa mashambulizi ya mitandaoni mwishoni mwa mwaka uliopita ambapo
michezo ya video ya Sony pamoja na Xbox ilipotea.
No comments:
Post a Comment