
Meneja wa
Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu
masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa
Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika
katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya
kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na
Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous leo

Maelezo kuhusu masalia hayo ya injini hiyo ya moshi iliyoachwa na wajerumani Benson Kibonge

Waziri
Nyalandu akitembela maeneo mbalimbali ya mbuga hiyo ya Selous kabla ya
kukabidhiwa vifaa hivyo ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya
wanyama ya Selous leo. anayemuongoza na Meneja wa mbuga hiyo


Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye alialikwa kwenye hafla hiyo, akitazama mto Ruaha unaopita katika mbuga ya Selous

Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza maneno ya Utangulizi kabla ya kukabidhiwa vifaa vya kukabiliana na ujangili kutoka na serikali za Marekani na Ujerumani katika hafla hiyo. Kulia ni Balozi wa Mrekani Mark Childress na waili kulia ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke

Balozi wa
Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana saini na
Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni Balozi wa
Ujerumani Egon Kochanke

Balozi wa
Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania,
Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa Tanzania
msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa wanyamapori na
vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori
ya Selous leo.

Waziri
Nyalandu akibadilishana hati na Balozi wa Marekani, Mark Childress baada
ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke

Waziri
Nyalandu akibalidilishana hati na Balozi wa Ujerumani Tanzania Egon
Kochanke, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujerumani kuipa Tanzania
msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika mbuga ya
wanyama ya Selous leo

Waziri
Nyalandu akimshukuru balozi huyo wa Ujerumani baada ya kubadilishana
hati walizosaini. kulia ni Balozi wa Marekani Tanzania Mark Childress


Waziri Nyalandu akitoa maelezo baada ya kutiliana saini na mabalozi wa Marekani na Ujerumani

Vifaa
mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani
kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyamapori ya
Selous

Askari
wa Wanyamapori Anita Albert akijaribu kionambali ambacho ni miongoni vya
vifaa vilivyotolewa kwa Tanzania na Serikali za Marekani na Ujerumani
kwa ajili ya kukabiliana na ujangili

Askari wa
wanyamapori wakikagua mahema ambayo ni miongoni mwa vifaa vya kisasa
vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya
kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous. Picha
zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment