Saturday, 31 January 2015

Mtaalamu wa silaha za kemikali IS auwawa






Jeshi la Marekani linasema kuwa mtaalamu mmoja wa silaha za kemilkali aliyekuwa akifanya kazi na kundi la Islamic State ameuawa kwenye mashambulizi ya muungano nchini Iraq.
Marekani inasema kuwa kifo cha mwanamume huyo kwa jina Abu Malik kitavuruga uwezo wa kundi hilo wa kuunda na kutumia silaha za kemikali.
Abu Malik anaripotiwa kufanya kazi kama mtaalamu wa silaha za kemikali kwa rais wa zamani wa Iraq Sadam Hussein kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani mwaka 2003.
Kundi la Islamic State hudhibiti maeneo makubwa nchini Syria ambapo serikali imekuwa ikiharibu silaha za kemikali.

Lazaro Nyalandu na Aunt Ezekiel Wachanwa Bungeni!!!



Lazaro Nyalandu na Aunt Ezekiel  Wachanwa Bungeni!!!



 Jana wakati mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema , akichangia  hoja Bungeni nakudai kuwa mawaziri wengi  hawana ubunifu nakumrushia “bomu”  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa anazunguka nje ya nchi na msichana kwa madai ya kutangaza utalii.
Lema alisema;
“Angalia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alikwenda kutangaza utalii nje ya nchi akiwa ameongozana na (mwigizaji maarufu wa filamu wa Tanzania) Anti Ezekiel,” alisema na kuongeza kuwa waziri huyo hashindi ofisini kwa kisingizio cha kutangaza utalii.
Picha za wawili hawa wakiwa nchini Marekani  wakitangaza utalii zilisambaa sana mtandaoni mwaka jana na kizua stori nyingi juu kile kilichofanyika.
Picha : Waziri Nyalandu akiwana Aunty Ezekiel pamoja na DJ Luke (wakatikati) wakitangaza Utalii, New York, Marekani.
Lakini hivi kuna ubaya gani Staa wetu kushirikiana na waziri katika kutangaza UTALIIII?!!



BARABARA YA KWENDA OLOLOSOKWAN YAWA TISHIO KWA MAGARI MAKUBWA

DSC_0035
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyemtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kikazi ya siku nne kwenye kijiji cha Ololosokwani na halmashauri ya Ngorongoro kwa ajili ya maandalizi ya mradi wa kijiji cha digitali unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Ki-elektronic ya Samsung unaotarajiwa kuwasili kijijini hapo mwezi februari ukitokea jijini Dar.
MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues ameonesha mashaka yake juu ya ubora wa barabara ambazo magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali Ololosokwan yanaweza kupita.
Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali wakati alipomtembelea ofisini kwake. Akiwa katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya kumwelezea shughuli za Unesco katika wilaya yake, Mkurugenzi Mkazi huyo alipata nafasi ya kuzungumzia haja ya kuboreshwa kwa maaneo kadha ya barabara kuelekea kijiji cha Olosokwan ili kuyawezesha magari hayo makubwa kufika kwa urahisi.
Huku akimuonesha mkuu wa wilaya baadhi ya picha alizopiga akiwa njiani kukagua njia ya kupita magari hayo na kuangalia maandalizi ya mwisho ya mradi huo mkubwa na wa kipekee nchini alisema hali ya barabara si nzuri hata kidogo. Vifaa kwa ajili ya kijiji hicho vipo bandarini tayari na magari yanayoweza kubeba makontena hayo ni makubwa na barabara za kuelekea kijiji hicho ni mbaya.
DSC_0041
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) aliyeambatana na wataalamu wa elimu, afya na mawasiliano pamoja na Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia (hayupo pichani) .
                                                                                                 VICTOR SIMON

PAC YAISHAURI SERIKALI NAMNA YA KUINUSURU KAMPUNI YA TTCL

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe wakiwa katika majukumu yao.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa katika majukumu.
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa mapendekezo ya kuinusuru Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kutokana na hali mbaya ya kampuni hiyo kifedha kwa sasa ambapo inaendeshwa kwa hasara huku ikiwa na madeni makubwa. PAC imetoa mapendekezo hayo katika taarifa yao kwa bunge ya mwaka juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mashirika ya umma iliyotolewa Januari 28 mwaka 2015.
Kwa mujibu wa taarifa ya PAC hali ya mapato na matumizi ya TTCL kwa mwaka 2012 ilipata hasara ya bilioni 20.883 huku kwa mwaka 2013 ikipata hasara ya bilioni 16.258. PAC ilisema majumuisho ya hasara ya TTCL kupata hasara kwa takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na hasara ambayo kwa mwaka 2013 ilifikia bilioni 334.48, jambo ambalo limeiondolea mvuto wa kukopeshwa na taasisi za fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.
"...Ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza miradi ya Kampuni umekuwa kikwazo kwa TTCL kukabiliana na ushindani wa kibiashara. Kwa kipindi kirefu ufanisi wa TTCL kiuwekezaji na kifedha umeendelea kudorora. Tangu TTCL ibinafsishwe mwaka 2001, hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika na mpango wa kutafuta mkopo kutoka mabenki ya ndani na nje ya nchi unakwamishwa na masharti ya kupata udhamini wa Serikali," ilieleza taarifa hiyo ya PAC. PAC iliongeza kuwa ukiacha madeni yaliopo pia TTCL inadaiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) jumla ya bilioni 25 hivyo kufanya jumla ya deni kufikia bilioni 101.6.
Kamati hiyo ya bunge imesema kuna umuhimu wa Serikali kufanya maamuzi ya haraka ya kuikwamua TTCL ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye Sekta ya Mawasiliano ikizingatiwa kuwa ndiyo inayoendesha Mkongo wa Taifa wa mawasiliano. Katika mapendekezo ya PAC ili kuikwamua TTCL imeishauri Serikali kununua hisa asilimia 35 zinazomilikiwa na Bharti Airtel katika TTCL kwa gharama ndogo kwani Bharti Airtel haikutimiza kikamilifu masharti ya mkataba wa mauziano ya hisa hizo hapo awali kwani tangu inunue hisa hizo haijafanya uwekezaji katika Kampuni ya TTCL.
"...TTCL isamehewe deni la Serikali Sh. 76.6 bilioni na deni la TCRA Sh. 25 bilioni ambayo jumla yake ni Sh. 101.6 bilioni na fedha hizo zipelekwe kuongeza mtaji ili Kampuni itoke kwenye kuwa na mtaji hasi wa Sh. 87.896 bilioni na kuwa na mtaji chanya wa sh. 13.704 bilioni. Likifanyika hili basi Kampuni hiyo itaweza kukopesheka. Serikali ikamilishe taratibu zake za kuimilikisha TTCL Mkongo wa Taifa ili izidi kuuendeleza kwa ufanisi na kuongeza mapato ya TTCL," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Hata hivyo PAC imeshauri kuwa kuna umuhimu wa kufanya marekebisho ya muundo wa Kampuni ya TTCL kwani kwa sasa ina idadi kubwa ya wafanyakazi (1549) isiyoweza kuwalipa.
Aidha, ilibainisha kuwa kwa sasa zinahitajika bilioni 32 kwa ajili ya kugharamia urekebishaji wa muundo wa Kampuni ili uendane na mahitaji ya utoaji wa huduma mbalimbali. Mashirika mengine yenye hali mbaya kifedha na uendeshaji ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania, ATCL ambayo kwa sasa ina madeni makubwa huku ikiwa na ndege moja aina ya Dash 8–Q 300, Wafanyakazi 142 na Jengo la ATC House lililoko mtaa wa Ohio, Dar es Salaam.

BUNGENI: CHENGE ACHARUKA KUHUSU UFISADI


MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ametakiwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha kauli yake ya kumtuhumu Mbunge Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), kwa ufisadi.
Chenge alilazimika kuomba utaratibu wa kiti juzi, baada ya Mbunge huyo wa Kawe kumtaja mara mbili wakati akichangia mjadala wa taarifa za kudumu za Bunge zilizowasilishwa juzi.
Mara ya kwanza, Mdee alimhusisha Chenge na mkataba mbovu wa Kampuni ya Ndege (ATCL) uliosababisha Serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh bilioni 90.
Licha ya kumtaja kwenye ufisadi huo ambao kwa mujibu wa Mdee, Chenge ndiye alikuwa Waziri wa Wizara yenye dhamana na ATCL, pia alimtaja kuhusika katika kashfa nyinginezo ikiwemo suala la utoaji takribani Sh bilioni 200, katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu (BoT).(P.T)
"Wabunge tuanze kuchunguzana humu ndani na kushughulikiana,"alisema Mdee na kutaja kwamba kwa kuanza, waanze na Chenge pamoja na Dk Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi), akimhusisha kuwa aliwahi kushika wizara hiyo yenye dhamana na ATCL.
Kauli hiyo ilimfanya Chenge kusimama na kusema; "kwa heshima zote nimemvumilia sana mheshimiwa (Mdee) anayechangia hoja hii. Kama ana ushahidi wa hayo anayosema, kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe mbele yako.
"Mimi ningelipenda Bunge hili liendelee kuwa na heshima yake. Pili naomba sana, hayo wanayoyasema wawe na ujasiri wa kwenda kuyasemea nje ya ukumbi huu wa Bunge, wasijifiche kwenye kinga ya Bunge.
"Nina mengi ya kusema, lakini kwa sababu nimesimama kwa hoja ya utaratibu, kunitaja moja kwa moja, naomba aweke hoja mezani,"alisema Chenge.
Mwenyekiti wa Bunge alikubaliana kwamba Mdee awasilishe ushahidi kwa kiti. Hata hivyo Mdee alijibu, "Kuna utaratibu wa kikanuni, vielelezo nikitakiwa kuleta nitaleta.
"Tunazungumza hapa matumizi mabovu, mikataba mibovu na wizi wa mali ya umma. Mzee wangu (Chenge) ni rafiki yangu lakini nimeamua nimfungukie kwa sababu haya ni mambo makubwa."

Friday, 30 January 2015

MUGABE ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA AU


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ndio mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika -Au
Rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka tisini, sasa ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa muungano wa Afrika-AU.
Wajumbe walimteuwa Mugabe kwa kauli moja katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Ababa-Ethiopia.
Sasa Mugabe amechukua mahala pak mwenyekiti anayeondoka wa muungano huo, Nkosazana Dlamini-Zuma.
Uteuzi wa Mugabe kuongoza muungano huo mkubwa ulio na wanachama zaidi ya arubaini, sasa umeingiza doa ndani ya AU, kwani Mugabe hana uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kukaa uongozini tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru mnamo mwaka wa 80.BBC



.

Umoja wa Afrika: mshikamano dhidi ya Boko Haram

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma ametangaza mjini Addis Ababa, Ethiopia kuundwa kwa kikosi cha kimataifa kwa kuanzisha vita dhidi ya Boko Haram.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma ametangaza mjini Addis Ababa, Ethiopia kuundwa kwa kikosi cha kimataifa kwa kuanzisha vita dhidi ya Boko Haram.
Na RFI
Uamzi wa pamoja umechukuliwa na Umoja wa Afrika wakati wa kikao chake cha Baraza la amani na usalama Alhamisi Januari 29 jioni mjini Addis Ababa, Ethiopia na kuhudhuriwa na zaidi ya marais kumi na tano.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan na rais wa Cameroon Paul Biya hawakushiriki kikao hicho. Umoja wa Afrika unaunga mkono kikosi cha kimataifa cha wanajeshi 7500.(P.T)
Lengo la Umoja wa Afrika ni kushawishi Umoja wa Mataifa kufadhili mashambulizi ya kikosi hicho cha Umoja wa Afrika.
Uamzi huo umechukuliwa na marais na viongozi wa serikali za Afrika Alhamisi 29 Januari mjini Addis Ababa, ambao wanakabiliwa na tishio la Boko Haram.
Mwezi ujao, Umoja wa Afrika utakutana rasmi na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ili kuliomba kusaidia, kupitia mfuko wa amani, msaada wa vifaa na fedha kwa kikosi cha kimataifa chenye wanajeshi 7500, ambao watatakiwa, kwa mujibu wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, kupambana dhidi ya Boko Haram.
Umoja wa Afrika unaunga mkono jitihada za jumuiya ya nchi zinazochangia Ziwa Chad, za kuundwa kwa kikosi cha kimataifa kutoka Nigeria, Chad, Cameroo, Niger na Benin.
Uamzi huu umechukuliwa na zaidi ya marais kumi na tano ambao ni wajumbe wa Baraza la amani na usalama, uamuzi ambao unatazamiwa kupitishwa katika mkutano mkuu wa marais na viongozi wa serikali ambao utadumu siku mbili kuanzia Ijuma wiki hii.
Nigeria na majirani zake wameafikiana juu ya msimamo wa pamoja, baada ya miezi ya kutoaminiana na kutokuelewana. Lakini kama Umoja wa Afrika, kupitia jumuiya ya nchi zinazochangia ziwa Chad, una wanajeshi, bao unakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya kijeshi na fedha.

SIMBA WAAMUA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU


WAZEE wa Simba wameona isiwe taabu na wameamua kurudi kazini kwa kufanya kikao chao cha dharura na baadhi ya viongozi na jana Alhamisi jioni walituma ujumbe wao kambini kuzungumza na wachezaji kwenye kikao cha faragha kutaka kujua tatizo ni nini mbona timu inayumba?
Lakini si hilo tu, viongozi wa matawi ya Simba Dar es Salaam wameungana na kuuandikia barua uongozi wakishinikiza mambo matatu ambayo ni uamuzi mgumu, ambayo ni kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama kujua tatizo la timu yao, kufumua benchi la ufundi abaki kocha Mserbia, Goran Kopunovic pekee na mwisho Kamati ya Mashindano ipigwe chini.
Wanachama hao chini ya kiongozi wao, Masoud Ustaadh, wanadai kwamba mambo hayo ndiyo tatizo na chanzo cha Simba kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu Bara na kwamba viongozi wa kamati wamekuwa wakiingilia benchi la ufundi.(P.T)
Kwa mujibu wa maelezo yao, wanataka hata Selemani Matola apigwe chini kwa madai kwamba hata Kocha Patrick Phiri alishadokeza awali kuwa Kocha Msaidizi huyo hafai.
Rais wa Simba, Evans Aveva, amekiri kupokea barua hiyo na kusema anaifanyia kazi kwa mujibu wa Katiba ya Simba.
Tafrani hiyo imezuka baada ya timu hiyo kupigwa mabao 2-1 na Mbeya City juzi Jumatano kwenye mechi ya ligi hiyo ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wazee hao waliibukia kambini jana kutaka wachezaji wawaambie ukweli ambapo kikao hicho kilitumia saa kadhaa huku kukiwa na usiri mkubwa.
Mmoja wa wachezaji aliiambia Mwanaspoti baadaye kwamba baadhi yao walitamka kwamba walifungwa kwa makosa ya uwanjani, ingawa wengine walilalamika kuwa morali iko chini kwavile viongozi hawapo karibu nao.
Kocha aliyetimuliwa na Simba, Patrick Phiri kwa upande wake ameweka wazi kwamba timu hiyo ilikosea kuwaacha Amri Kiemba na Haroun Chanongo lakini akatoa angalizo kwamba Mserbia Kopunovic asiguswe, aachwe afanya kazi yake.
Phiri alitimuliwa Simba mwezi uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Mserbia huyo.
Akizungumza na Mwanaspoti jana kutoka Zambia, Phiri alionyesha kusikitishwa na matokeo ya Simba lakini akasema: "Bado uwepo wa Chanongo na Kiemba ndani ya Simba ulikuwa muhimu sana, kila mchezaji ana udhaifu wake kama binadamu, lakini viongozi wanapaswa kukaa na wachezaji kuzungumza nao kujua matatizo yao."
Kiemba alijiunga na Azam kwa mkopo kama Chanongo alivyokwenda Stand United ya Shinyanga.
"Simba haina wachezaji wengi wenye uzoefu, waliopo ni wazuri lakini hakuna umoja wa dhati, bado kuna makundi kwa wachezaji, viongozi waangalie hili kwa kina, ijapokuwa matokeo yanaumiza sana na nimekuwa nikifuatilia Simba kwa karibu," alisema Phiri
"Kwa sasa wasije kufanya kosa la kumfukuza kocha, wakae waangalie wapi kuna tatizo ndani na nje ya timu, bado wana nafasi ya kufanya vizuri bado mechi ni nyingi."
Mzungu amshangaa Chollo
Kopunovic ameshangazwa na tukio la beki mkongwe kuamua kupiga penalti ambayo iliwanyima sare dhidi ya Mbeya City, lakini akatamka kwamba kupoteza mchezo huo ni vizuri kwa sasa kwa sababu itawashtua na kuwarudisha mchezoni kwavile wachezaji walishaanza kujisahau.
"Sawa, sikuwahi kusema nani apige penalti ya kwanza katika mechi zetu, lakini Chollo kupiga penalti lilinishangaza sana kwa kuwa ukiacha mazoezini sikuwahi kumuona akipiga penalti katika mechi lakini sitaki kumlaumu sana," alisema Kopunovic akizungumzia penalti iliyokoswa na Nassor Masoud 'Chollo' na kuipa Mbeya City ushindi wa mabao 2-1.
"Angalia tulivyocheza dakika 30 za mwisho, kwa namna moja nafurahia haya matokeo unajua tangu tuchukue Kombe la Mapinduzi wachezaji wangu walijisahau walikuwa wanajiona wao mastaa wakubwa ni kama wamechukua ubingwa wa ligi, hapa sasa wataamini kuwa safari yao bado ni ndefu."

Tuesday, 27 January 2015

TAARIFA MTANDAO WA FACEBOOK KUPOTEA DUNIANI KWA DAKIKA 40

TAARIFA MTANDAO WA FACEBOOK KUPOTEA DUNIANI KWA DAKIKA 40

Mtandao wa kijamii wa facebook ulikuwa hauingiliki katika maeneo mengi duniani mapema leo kabla ya huduma zake kurudi.
Mamilioni ya watumizi wa mtandao wa facebook walishindwa kuingia katika akaunti zao.
Wateja wake katika mataifa mengine walishindwa hata kutumia hudumu ya Instagram.
Facebook ilisema kuwa wahandisi wake ndio walioababisha tatizo hilo, na kukana madai kwamba kundi moja linalotekeleza uhalifu wa mitandaoni lilihusika.
''Awali watu wengi walikuwa hawawezi kuingia katika akaunti zao za mitandao ya facebook pamoja na huduma ya Instagram'', msemaji wa facebook aliiambia BBC.
''Hili halikuwa shambulizi kutoka kwa watu wengine lakini lilitokea baada ya kufanya mabadiliko ambayo yaliathiri mpangilio wa mfumo wetu''.
Tuliharakisha na kutatua tatizo hilo na sasa huduma zote zimerejelea asilimia 100 kama kawaida
Mitandao hiyo ilitoweka kwa takriban dakika 40 kabla ya kurudi.
Programu ya mtandao unaowaunganisha wapendanao Tinder ambayo hutegemea facebook ili kutoa huduma zake pia iliathiriwa na tataizo hilo.
Kundi moja la uhalifu wa mitandano kwa jina Lizard Squad liliandika ujumbe kwa twitter kuhusu hudumu hiyo kutoweka na kusababisha ripoti kwamba huenda lilihusika.
Kundi hilo limeshtumiwa kwa mashambulizi ya mitandaoni mwishoni mwa mwaka uliopita ambapo michezo ya video ya Sony pamoja na Xbox ilipotea.

Saturday, 24 January 2015

MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI HAYA HAPA

JKLeo huenda ikawa moja ya siku ambayo itaingia kuwa siku yenye headlines kubwa kwenye siasa TANZANIA, wakati wa mchana kulikuwa na taarifa kutoka Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dar es Salaam ambapo aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo alifanya kikao na waandishi wa Habari na kutangaza kujiuzulu.
Kubwa nyingine kwenye upande huo huo ni ishu ya Rais Kikwete kutangaza mabadiliko madogo ndani ya Baraza la Mawaziri, ambapo mabadiliko hayo nimekuwekea hapa, wapo waliohamishwa na wapo waliokuwa Manaibu Mawaziri sasa ni Mawaziri, list yote ni hii hapa;
Mawaziri
George Simbachawene – Waziri wa Nishati na Madini
Mary Nagu- Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais- Mahusiano na Uratibu
Christopher Chiza- Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
Harrison Mwakyembe- Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
William Lukuvi- Waziri wa Ardhu, Nyumba na Makazi
Steven Wasira- Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Samuel Sitta- Waziri wa Uchukuzi
Jenista Muhagama- Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge
Manaibu Waziri
Stephen Masele- Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais- Muungano
Angela Kairuki- Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi
Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Anna Kilango- Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Charles Mwaijage- Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Friday, 23 January 2015

Abiria wahofia usalama wa Kivuko cha Mv. Magogoni

23rd January 2015

Kivuko cha Mv. Magogoni
 
Wakazi wa Feri, Dar es Salaam, wameiomba Serikali kukifanyia marekebisho kivuko cha MV Magogoni kinachofanya safari zake kati ya Kivukoni na Kigamboni  ambacho kimekuwa kilaharibika kila mara na kusababisha usumbufu kwa abiria.
 
Hatua hiyo imefuatia matukio ya kuharibika mara kwa mara nyakati za usiku na kuchukua  muda majini huku kikiwa na abiria na magari.
 
Fadhili Mbaga, mkazi wa Kigamboni,  alisema, Serikali  inapaswa kuangalia kwa makini suala la usalama wa abiria wa Feri ambao wanatumia usafiri huo, kutokana na kivuko hicho kutokuwa na sifa za kusafirisha abiria wengi na mizigo kwa wakati.
 
 “Abiria tumekuwa na wasiwasi na huu usafiri kwani mara nyingi injini ya kivuko hiki siyo nzima na kusababisha ofu kubwa kwetu,” alisema.
 
Anna Mwasombe, mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere, alisema kutokana na ubovu wa kivuko hicho, abiria wengi wasiokuwa na haraka hulazimika kusubiri kupanda kivuko cha MV Kigamboni.
 
“Mara nyingi  kivuko hiki kikiwa kinafanya safari zake hutumia saa nyingi kufika upande wa pili kutoka na kuelemewa, hivyo kusababisha abiria kutumia muda mrefu kufika kutokana na kutembea taratibu,” alisema.
 
Samson Gama, alisema Serikali kwa kushirikiana na Wakala wa Ufindi na Umeme (Temesa) inapaswa kufanya ugaguzi  kila wakati ili kuhakikisha vivuko  vyote vinakuwa katika hali nzuri  na salama kusafirisha abiria.
 

Jambazi atupwa jela miaka 45

Jambazi atupwa jela miaka 45

23rd January 2015

Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga, justus kamugisha.
Kinara wa mtandao wa ujambazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Njile Samuel (46) maarufu John, amehukumiwa kifungo cha miaka 45 jela pamoja na kulipa faini ya Sh. milioni tatu baada ya kukiri makosa yote mawili yaliyokuwa yakimkabili.
 
Mshtakiwa huyo alihukumiwa kosa la kwanza kifungo cha miaka 15 jela na faini ya Sh. milioni tatu mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Robert Oguda, baada ya kusomewa mashitaka yake.
 
Ilidaiwa katika shitaka la kwanza, Januari 10, mwaka huu, saa 9:00 alasiri, eneo la Lyoma wilayani Bariadi, Njile alikamatwa na risasi 272, bunduki aina ya SMG na magazini saba.
 
Katika shitaka la pili lililosomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Aidan Mwilapa, mshtakiwa huyo alihukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa kupatikana na bunduki, huku kosa lingine alihukumiwa kifungo kama hicho kwa kupatikana na umilikaji wa silaha bila kibali.
 
Hata hivyo, adhabu hizo zitakwenda kwa pamoja na mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.
 
Wiki iliyopita, Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, walikutana jijini Mwanza na kumuelezea Njile ni jambazi hatari ambaye katika kazi yake alikuwa akiwaua wenzake baada ya kufanya uhalifu.

IDRIS WA BBA AZAWADIWA BONGE LA NYUMBA NA BOS WAKE

  Friday, 23 January 2015

IDRIS WA BBA AZAWADIWA BONGE LA NYUMBA NA BOS WAKE

Ama kweli mwenye nacho ndio huongezewa,... Mshindi wa BBA 2014 kutoka Tanzania, Idris Sultan ambae kwa sasa anamiliki dola za kimarekani lakini 3 alizoshinda kupitia BBA.

 kijuzi
Idriss amekabidhiwa mjengo unaouona hapo juu na boss wake ambae pia ni mmiliki wa kampuni ya ALOSCO "Ghalib"
Mjengo huo upo maeneo ya Mbenzi Beach na Idris yupo tayarai kwa ajili ya kuhamia weekend hii (Jumapili)
http://kijuzi.blogspot.com

Thursday, 22 January 2015

TIZAMA VIDEO YA Y TONY FT BARNABA- MAMA

TIZAMA VIDEO YA KAKA JAY, TANZANIA HAPA

MAREKANI NA UJERUMANI WATOA VIFAA VYA KISASA KUKABILIANA NA UJANGILI MBUGA YA SELOUS


Meneja wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous leo

Maelezo kuhusu masalia hayo ya  injini hiyo ya moshi iliyoachwa na wajerumani Benson Kibonge

Waziri Nyalandu akitembela maeneo mbalimbali ya mbuga hiyo ya Selous kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyama ya Selous leo. anayemuongoza na Meneja wa mbuga hiyo
Waziri Nyalandu akisalimiana na Ofisa Mawasiliano na Umma wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,  David Feloemann, alipowasili kwenye mbuga ya Selous leo(P.T)

Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye alialikwa kwenye hafla hiyo, akitazama mto Ruaha unaopita katika mbuga ya Selous

Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza maneno ya Utangulizi kabla ya kukabidhiwa vifaa vya kukabiliana na ujangili kutoka na serikali za Marekani na Ujerumani katika hafla hiyo. Kulia ni Balozi wa Mrekani Mark Childress na waili kulia ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke

Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana saini na Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani  Egon Kochanke

Balozi wa Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa Tanzania msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa wanyamapori na vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous leo.

 Waziri Nyalandu akibadilishana hati na Balozi wa Marekani, Mark Childress baada ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke

 Waziri Nyalandu akibalidilishana hati na Balozi wa Ujerumani Tanzania  Egon Kochanke, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujerumani kuipa Tanzania msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyama ya Selous leo

 Waziri Nyalandu akimshukuru balozi huyo wa Ujerumani baada ya kubadilishana hati walizosaini. kulia ni Balozi wa Marekani Tanzania Mark Childress


 Waziri Nyalandu akitoa maelezo baada ya kutiliana saini na mabalozi wa Marekani na Ujerumani

 Vifaa mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous

 Askari wa Wanyamapori Anita Albert akijaribu kionambali ambacho ni miongoni vya vifaa vilivyotolewa kwa Tanzania na Serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili

Askari wa wanyamapori wakikagua mahema ambayo ni miongoni mwa vifaa vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog 

TAMBWE ASIMULIA ANAVYOTESWA,YANGA YASHITAKI

muro 2
Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya manyanyaso anayoyapata.
Akizungumza mchana huu katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa Tambwe wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo wanataka mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua kali wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka shirikisho hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa mchezo huo lengo likiwa ni kujua umakini wa waamuzi hao.(P.T)
muro
“Tatu tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia kuwachukulia hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa kubaini haya ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana wafungiwe na Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo tutagoma na hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi wao kushabikia maovu haya.
Aidha Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema ameshangazwa kuona anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi kuyaweka hadharani.
“Mpira ni starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani unanikaba hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu wanajua maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo kiungwana siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema Tambwe

Vurugu zazuka upya Donetsk

Kwa uchache watu 13 waliuawa katika shambulio dhidi ya gari katika mji wa Donetsk, Alhamisi Januari 22 mwaka 2015.
Kwa uchache watu 13 waliuawa katika shambulio dhidi ya gari katika mji wa Donetsk, Alhamisi Januari 22 mwaka 2015.
Na RFI
Watu thelathini na wanne wameuawa ndani ya masaa 24 Mashariki mwa Ukraine. Hata hivyo wito wa kusitisha mapigano uliyotolewa Jumatano Januari 21 mjini Berlin na Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani, Urusi, na Ukraine umepuuzwa.
Shambulio baya lililosababisha maafa makubwa limetokea Alhamisi Januari 22 asubuhi katika mji wa Donetsk, Mashariki mwa Ukraine. Shambulio hilo limegharimu maisha ya watu 13, baada ya gari waliokuwemo kushambulio kwa bomu.(P.T)
Shambulio limetokea katika kata ya Kusini Magharibi mwa Donetsk, kata ambayo ilikua bado haijaguswa na mapigano. Gari waliyokuwemo watu hao limeteketea.
Waangalizi wa jumuiya inayohusika na usalama na ushirikiano barani Ulaya wamefika eneo la tukio ili kujaribu kujua sababu za shambulio hilo.
Jeshi la Ukraine na waasi mara mara, wamekua wakitupiana lawama na kunyoosheana kidole kuhusika na shambulio hilo.
Ikijaribu kujitetea, Wizara ya ulinzi ya Ukraine imethibitisha kwamba eneo kulikotokea shambulio ni kwenye umbali wa kilomita 15 na eneo kunakopatikana askari wa Ukraine.
Jeshi limepata pigo kubwa kwa mashambulizi hayo yanaoendelea Mashariki mwa Ukraine. Wanajeshi kumi wa Ukraine waliuawa saa 24 zilizopita, huku askari wakiondoka katika uwanja wa Donetsk, na kwa sasa uwanja huo unadhibitiwa na waasi.
Waziri mkuu wa Ukraine ameishtumu Urusi kuhusika katika shambulio dhidi ya gari hilo liliyotokea leo Alhamisi na kusababisha vifo vya watu 13. Kwa upande wake, Urusi umelinyooshea jeshi la Ukraine kuhusika na shambulio hilo.

Serikali yakana kuwaua waandamanaji DRC

Serikali inasema kwamba walinzi wa maduka binafsi ndio waliowaua waandamanaji

Serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekanusha madai ya kuwauwa waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga mapendekezo ya kubadilisha sheria za uchaguzi mkuu.
Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu arubaini wameuawa katika siku tatu za ghasia.BBC
Waziri wa mawasiliano Lambert Mende, aliambia BBC kwamba polisi hawakutumia silaha zozote dhidi ya waandamanaji hao.
Alisema waandamanaji ambao aoliwataja kama waporaji, waliuawa na walinzi waliokuwa wanalinda majengo ya biashara yaliyoporwa
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kwamba zaidi ya watu 40 wameuawa katika siku tatu za vurugu mjini Kinshasa.
Mabadiliko yaliyopendekezwa huenda yakachelewesha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao, wakati Kabila anatarajiwa kung'atuka baada ya kuitawala nchini huo kwa miaka 14.

Wednesday, 21 January 2015

ZITTO AMWAGA MACHOZI UKUMBINI

 ZITTO AMWAGA MACHOZI UKUMBINI

Hakika wikiendi iliyopita ilikuwa ni shangwe tupu, lakini kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia leseni ya Chadema, Zitto Zuber Kabwe ilikuwa ya machungu pale alipojikuta akimwaga chozi ukumbini.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia leseni ya Chadema, Zitto Zuber Kabwe akiwa na Christian Bela.
Mpango mzima ulioshuhudiwa na paparazi wetu ulijiri kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo Bendi ya Malaika, chini ya Christian Bella ilikuwa ikishusha burudani ya kufa mtu.
Wakati Mbunge wa Jimbo la Sikonge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Said Nkumba alitesa kwenye jukwaa la Msondo Ngoma pale TTC Chang’ombe, Temeke, Zitto alifunika vibaya Mango Garden, Kinondoni, kwani alikuwa zaidi ya shabiki, pedeshee na mwimbaji.
Katika muda ambao watoto wa mjini husema ni usiku mnene, Zitto ambaye yupo katika mgogoro na chama chake, alipanda jukwaani wakati prezidaa wa Malaika Band, Christian Bella ‘Obama’ akiimba wimbo wake mpya wa ‘Nani Kama Mama’ ambapo mheshimiwa huyo alichotwa na hisia za kibao hicho hadi kujikuta akimwaga machozi kwa kumbukumbu ya msiba wa mama yake mzazi uliotokea mwaka jana (Shida Salum, alifariki Juni 1, 2014 jijini Dar es Salaam).

Mh. Zitto Kabwe akiteta jambo na wanamuziki wa Bendi ya Malaika.
“Lilikuwa ni tukio la kushangaza kwa mheshimiwa, maana alipanda stejini kisha akajiunga na waimbaji, akachukua gitaa na kuanza kucharaza kana kwamba alifanya nao mazoezi,” alisema shabiki mmoja ukumbini hapo,
Hata hivyo, baadaye mwanasiasa huyo kijana kipenzi cha wengi, aliimarika na kuendelea kuuimba wimbo huo huku akiserebuka kwa kwenda mbele.
Baada ya kuona hivyo, mashabiki walimiminika jukwaani kupiga naye picha kwa muda wa takriban dakika 20, ambapo mbunge huyo alithibitisha kuwa ni mtu wa watu kwani shughuli zote zilisimama kwa muda ukumbini humo.

Katika hali hiyo, mapedeshee, ambao hung’ara katika kumbi kwa kutunza waimbaji na wanenguaji, walizimwa ngebe zao kwani Zitto alifunika kwa kutoa ‘mshiko’ wa kufa mtu.
Ilifahamika kwamba, Bella peke yake alipokea zaidi ya noti 50 za elfu kumi-kumi za Kitanzania kutoka kwa Zitto huku nyingine zikiwa ni dola za Kimarekani.

Wakipiga picha ya pamoja.
Hata hivyo, katika hali nyingine, baadhi ya watu walihoji usalama wa Zitto kuwa ni sawa na sifuri katika kipindi hiki ambacho bado sakata la kashfa ya uchotwaji wa mabilioni kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta linaendelea kushika kasi na vigogo kufikishwa mahakamani.
Watu hao walisema kwa namna Zitto alivyoingia ukumbini hapo na kujichanganya na mashabiki, ni rahisi kwa mtu mwenye nia mbaya kuweza kumdhuru, hasa watu wa Escrow ambao wana mapesa yanayoweza kuwashawishi kumfanya lolote.
“Watu wanatetemeshwa na hili skendo, leo wakimuona Zitto hapa kajiachia namna hii, watakumbuka jinsi alivyosimama kidete bungeni kutaka waliohusika wawajibishwe na fedha zirudishwe, unadhani nani hajui utamu wa fedha,” alisikika shabiki mmoja akisema.
Zitto alitafutwa kupitia simu yake ya mkononi ili kupata maoni yake juu ya usalama wake, lakini iliita bila kupokelewa.

Mshtakiwa Tegeta Escrow aachiwa kwa dhamana

Mshtakiwa Tegeta Escrow aachiwa kwa dhamana


MSHITAKIWA ESCROW ALIYEACHIWA KWA ZAMANA
Meneja wa Misamaha ya Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kyabukoba Mutabigwa.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwachia kwa dhamana Meneja wa Misamaha ya Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kyabukoba Mutabigwa, anayatuhumiwa kupokea zaidi ya Sh. bilioni moja kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow baada ya kutimiza masharti.

Mshtakiwa huyo alitimiza masharti mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.

Ijumaa iliyopita, Mtabingwa alipandishwa kizimbani na kutakiwa kuwasilisha mahakamani fedha taslim Sh. bilioni moja ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo, wadhamini watatu watakaosaini hati ya  dhamana ya maandishi ya Sh. milioni 340 kila mmoja, wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi zinazotambulika na kutotoka nje ya Jiji la Dar es Salaam bila kibali.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti hayo na kupelekwa mahabusu hadi jana alipokamilisha hati tano za mali zisizohamishika zenye thamani ya Sh. bilioni 1.3 na wadhamini watatu, wawili wafanyakazi wa TRA na mmoja mjasiriamali.

Katika kesi ya msingi, Mutabingwa anakabiliwa na mashitaka manne anayodaiwa kutenda Januari 27, 2014 maeneo ya Benki ya Mkombozi iliyopo Manispaa ya Ilala.

Inadaiwa mshtakiwa akiwa katika wadhifa wake wa Meneja wa Misamaha ya Kodi wa TRA, alipokea rushwa ya Sh. 1, 617,000,000  kupitia akaunti namba 00110202613801 kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engineering na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL, James Rugemalira.

Fedha hizo ni miongoni mwa zilizokuwamo katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Mshtakiwa anadaiwa kupokea tuzo hiyo kwa kuwawakilisha TRA na Mabibo Beer Wines and Spirits inayomilikiwa na Rugemalira.

Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, alidai katika shitaka la pili kuwa, Julai 15, mwaka jana, maeneo ya Benki ya Mkombozi, mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh 161,700,000 kupitia akaunti namba 00110202613801, fedha za Escrow kutoka kwa Rugemalira.

Katika shitaka la tatu, inadaiwa kuwa Agosti 26, mwaka jana, maeneo ya Benki ya Mkombozi, mshtakiwa alipokea tena rushwa ya Sh. 161,700,000 kupitia akaunti hiyo hiyo kutoka kwa Rugemalira na  fedha hizo zilikuwa katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Swai, alidai katika shitaka la nne kuwa Novemba 14, mwaka jana, kwa kutumia akaunti yake hiyo, alipokea rushwa ya Sh. 161,700,000 kutoka kwa Rugemalira, fedha ambazo zilikuwemo katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Kesi hiyo itaanza  kusikilizwa Januari 29, mwaka huu

Kituo cha Polisi Ikwiriri Chavamiwa na Majambazi, Askari wawili Wauawa, Bunduki, Risasi zaporwa


Majambazi yaliyojihamu kwa silaha yamevamia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua askari wawili na kupora silaha zilizokuwepo kituoni hapo.
  
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na WP Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
 
Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika tukio la uvamizi, kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani.
 
Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabomu ya machozi na risasi 60 za SMG.

Tabia Kuu Tano Za Watu Waliofanikiwa Kimaisha!

Kwanza, kabla sijaendelea embu tuwekane sawa kuhus hii falsafa ya “kufanikiwa kimaisha”, ina maana gani haswa? Ukweli ni kwamba watu wengi wakisikia fulani amefanikiwa kimaisha, basi moja kwa moja wanafikiri au wanaamini mtu huyo atakuwa na pesa nyingiiii au kwa maneno mengine, mtu huyo ni tajiri fulani hivi. Pamoja na kwamba pesa ndio mtatuzi wa mahitaji mengi hapa duniani, lazima tukumbuke kwamba pesa ina uwezo wa kununulia kitanda cha gharama kubwa sana, lakini ukashindwa kulala katika kitanda hicho kwa msongo wa mawazo. Pia pesa inaweza ikakufanya uopoe mwenza mzuri kuliko wote duniani, lakini mwenza huyo asiwe na mapenzi ya dhati kwako.
Hapa tunajifunza kwamba ingawa pesa ni muhimu sana maishani, kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mtu kimaisha hakuwezi kupimwa kwa kiasi tu cha pesa alichonacho. Mtu anaweza akawa na pesa, lakini akakosa raha kutokana na ukosefu wa amani ya ndani na nje ya mwili. Hivyo basi, Kufanikiwa au kutofanikiwa maishani kwa mtu, ni lazima pia kupimwe kwa mambo mengine muhimu kama uchamungu, ukarimu, maadili, busara, uvumilivu, na ujasiri (wa kufanya na kuishi na maamuzi magumu). Hivi “viambatanisho” 6 vya pesa ndio vinarutubisha na kudumisha pesa, na zaidi humfanya mtu afurahie (enjoy) pesa hizo. Kwa uzoefu wangu, mchanganyiko wa mambo haya yote muhimu, ndio humfanya mtu “afanikiwe kimaisha” kwa maana pana ya falsafa hiyo. Baada ya muhtahsari huu, tuendelee sasa na mada yetu, ambayo leo inagusia mambo makuu matano ya watu waliofanikiwa kama ifutavyo:
Bahari Zenji
#1: Huishi Kwa Siku Za Baadae (Future), Na Sio Siku Zilizopita (Past). Bila shaka umeshasikia ule usemi wa siku nyingi kwamba “yaliyopita si ndwele, tugange yajayo”. Watu waliofanikiwa kimaisha huwa na tabia ya kutokatishwa tamaa na mambo ambayo yameshapita, na hayakwenda kama walivyotarajia, kwani siku zote huwa wanakubali matokeo ya kutofanikiwa kwao katika suala fulani na kujipanga upya kulikabili suala hilo. Siku zote hujizuia kuruhusu matukio ya kushindwa kwao kufanikiwa katika masuala fulani maishani, kushusha imani yao yakufanikiwa katika masuala ya baadae (future).
amelelax
#2: Hawalii Shida Na Wala Hawana Kinyongo.  Hisia zako za siku kwa kiasi kikubwa zinategemea na wapi ulipoelekeza mawazo yako. Kwa mujibu wa mtaalam wa Saikolojia, Travis Bradberry, anaweka wazi kwamba “kama umeelekeza mawazo yako kwenye shida ambazo zinakukabili, basi unajijengea hisia hasi mwilini na kujiongezea mastresi kibao, ambayo yana athiri na kuzuia uwezo wako wa kufanya mambo ya kimaendeleo”. Hivyo basi, watu waliofanikiwa maishani huwa wanaelekeza mawazo yao kwenye masuala chanya, ili kupiga vita mastresi na kujiongezea uwezo wa kukomaa na mambo ya maendeleo. Pia, watu waliofanikiwa maishani huwa hawaendekezi kinyongo, kwani wanaelewa kuwa kuweka kinyongo katika masuala yaliyopita ni hatari sana kwa maendeleo. Vinyongo kama ilivyo kubebea shida mbeleko, ni vitu ambavyo huzalisha hisia hasi mwilini na kumfanya mtu kuwa na mastresi (au msongo wa mawazo), ambayo yana mzuia kufanya mambo ya maendeleo.
perfection
#3: Hawatoi Kipaumbele Katika Ukamilifu. Hapa ina maanisha kwamba, watu waliofanikiwa maishani huwa hawapotezi muda katika kutafuta ukamilifu (perfection) katika mambo yao. Ni watu, ambao wanafaham kwamba binaadam ni viumbe dhaifu na ukamilifu ni wa Mungu peke yake. Hivyo basi, hii sifa inawasaidia sana linapokuja suala la kuridhika na kile walichoweza kufanya baada ya kujitahidi kwa uwezo wao. Hii inawafanya waendelee kujiamini, badala ya kujilaumu na kujihisi wamefeli kama wale watu wanaolenga ukamilifu katika ufanyaji wa mambo yao.
Negative people
#4: Hawapotezi Muda Wao Na Watu Wenye Mawazo Hasi. Hii sifa ni muhimu sana na kwa ufupi ni muendelezo wa sifa #2, kwani ili mtu aendelee kubaki na mawazo chanya kwa mustakbali mzima wa maendeleo yake, ni lazima apinge kukaa na watu wenye mawazo hasi au walalamikaji. Kwa ung’eng’e wanasema “ don’t hangout with negative people!” Hapa wanazungumziwa marafiki, ndugu, na jamaa, yaani kuwa makini sana kuhusu watu unaokaa na kuzungumza nao kwa siku. Kama watu hawa wamejaa malalamiko tu kuhusu maisha yao siku nzima, basi jua wanagonjwa hatari sana na ni watu wa kukaa nao mbali, ili wasikuambukize gonjwa hilo hatari kwa maendeleo yako. Siku zote watu waliofanikiwa maishani (au wale walio mbioni kufanikiwa) huwa wanajihusisha na watu wenye mawazo chanya na matumaini tele kuhusu mustakbali wa maisha yao.
man-saying-no
Anza kufanya uchunguzi wako leo kwa watu unaowafaham, ambao “wamefanikiwa maishani” na utaona mifano hai ya sifa hizi au kama tayari unawafaham watu wao, basi tupe maoni yako kwa faida ya wasomaji wote!

CHANZO:THE HABARI

video mpya ya avril na ommy Dimpoz