Monday, 21 September 2015

Hii ni Top 10 ya warembo wa mastaa wa Ligi Kuu soka Uingereza 2015

Tumezoea kuona mastaa kadhaa wa soka kuingia katika headlines na wapenzi wao, wakiwa wametoka out katika sehemu mbalimbali za starehe baada ya kazi nzuri walioifanya uwanjani. Stori kutoka talksport.com waliwahi kutoa May 2015 list ya Top 10 ya warembo wa mastaa wa soka wa Ligi Kuu Uingereza.
10- Edurne Garcia huyu ni mpenzi wa golikipa wa klabu ya Manchester United David de Gea.
edurne_getty
De-Gea1



9- Lorena Bernal huyu ni mke wa kiungo wa Arsenal Mikel Arteta
lorenabernal_getty
bernal-and-arteta
8- Anara Atanes huyu ni mpenzi wa kiungo wa klabu ya Manchester City Samir Nasri
275CB7BF00000578-3030034-image-m-13_1428482498503
anara-atanes-et-samir-nasri-exact-353970864
7- Helen Flanagan mpenzi wa staa wa soka wa klabu ya Aston Villa Scott Sinclair
flanagangetty
C_71_article_1461799_image_list_image_list_item_1_image
6- Coleen Rooney mke wa mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney
rooney_getty
English soccer player Wayne Rooney and his girlfriend Colleen McLoughlin arrive for the FIFPRO World X1 Player Awards at the BBC TV centre, London, Monday Sept. 19, 2005.  The awards are taking place for the first time, and are the first  soccer awards voted by professionals from across the world.  (AP Photo/Kirsty Wigglesworth)
5-  Sam Cooke mpenzi wa beki wa kati wa klabu ya Manchester United Chris Smalling
sam-cooke
cooke_getty
4- Georgina Dorsett mpenzi wa kiungo wa zamani wa timu ya Manchester United na Everton Tom Cleverley
dorsett_getty
b93394d8f669b427f347c7afef75d5f4
3- Ludivine mrembo wa beki wa zamani wa klabu ya Arsenal na Manchester City Bacary Sagna
sagnagetty
France's defender Bacary Sagna and Ludivine Sagna enjoy a day out on a beach in Rio de Janeiro during the 2014 FIFA World Cup on June 26, 2014. AFP PHOTO / FRANCK FIFE        (Photo credit should read FRANCK FIFE/AFP/Getty Images)
2- Abbey Clancy mrembo wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Stoke City Peter Crouch
gettyimages-452325248
Abbey-Clancy-and-Peter-Crouch
1- Misse Beqiri mrembo wa golikipa wa zamani wa Man United ambaye ametimkia West Bromwich Albion msimu huu Anders Lindegaard.
Misse-Beqiri

Baada ya siku 40: sura ya mtoto wa Diamond na Zari ndio hii imeonyeshwa kwenye picha !

Zimeshatimia siku 40 toka mtoto wa Diamond Platnumz na Zarinah Hassan azaliwe, anaitwa Tiffah…. ambapo siku hii kubwa ilikumbukwa na nyumbani kwa Diamond watu mbalimbali wakaalikwa kama ilivyo kwenye utaratibu.
T2
T3
T1Picha zote 3 za juu ni kutoka kwenye Instagram page ya @8020fashions
T6
T7Ustaa wa Diamond Platnumz na Zari umeshawishi mpaka kampuni kubwa za kibiashara kuingia mkataba wa malipo kutumia jina na picha za Tiffah kibiashara ambapo mtoto huyu ambaye ndio kwanza katimiza siku 40 za kuzaliwa, tayari ni balozi wa maduka ya nguo za watoto Dar es salaam lakini pia picha yake ya kwanza imeonyeshwa ikiambatana na udhamini wa benki.
t9
t8

Mtoto wa Beckham amelikataa soka? Haya ndio maneno yaliyomuumiza baba yake

David Robert Joseph Beckham ni staa wa Soka ambaye kastaafu Soka na kuacha Rekodi kubwa na nzuri zinazoheshimika Duniani, yako maneno kwamba maji hufuata mkondo, mtoto wa Beckham na Soka la Baba yake je?
Stori ni vice versa, David Beckham kathibitIsha kwamba mtoto wake na Mchezo wa Mpira wa Miguu hata haviendani >>> “Mwanangu mmoja aliniambia kwamba haoni kama atakuja kuwa Mchezaji wa Mpira wa Miguu kwenye maisha yake, ilinivunja moyo kwa upande mwingine“- David Beckham.
BECKHAM_main_1473299a
Beckham akiwa na Familia yake kwenye matembezi yao.
Kwenye sentensi nyingine Beckham anasema mtoto wake ana hofu kwamba wapo watakaolinganisha kiwango chake na baba yake >>> “Kila nikiingia uwanjani najua watu wanasema ‘yule ni mtoto wa Beckham’, nisipokuwa na kiwango kizuri kama wewe hata haipendezi“- David Beckham.
David-and-his-sons

Tyga matatani na malimbukizi ya kodi, makosa ya kuvunja mkataba & wizi…!!





Hiko sio kitu pekee ambacho Jimbo la Carlifonia linataka kutoka kwa rapper huyo, mwezi uliopita Mahakama ilimuamuru Tyga kumlipa mwenye nyumba wa nyumba aliokuwa anaishi kodi ya nyumba ya miezi miwili ambacho kiasi chake kiligonga Milion 140 kwa pesa ya Kitanzania.
tyga6
Muonekano wa ndani wa duka la Tyga ‘Last Kings’.
Mengine ambayo Jimbo hilo linashitaki dhidi ya Rapper huyo wa Cash Money Records ni kesi ya kuvunja mkataba wake na moja ya club ya Las Vegas, mkataba ulikuwa wa dola 100,000 na ulikuwa unasema kwamba Tyga hatokuwa na mamlaka ya kuperfom sehemu yoyote ile Las Vegas isipokuwa club ya ‘Body English’ jijini humo, Tyga alivunja mkataba huo ambao kwa shilingi ya Kitanzania tunazungumzia makubaliano yaliozidi Milion 200 kwa kwenda kutoa show kwenye club nyingine jijini Las Vegas!

Sunday, 1 February 2015

Amuua mke kwa kumkata kichwa gesti

1st February 2015
Mkazi wa Tabata Mawenzi, Remi Joseph (36) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumkata kichwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends Corner ya jijini Dar es Salaam.
Aliyeuawa ni Josephena Moshi (35), ambaye alikatwa kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani wakiwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends Corner.

Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa  Kinondoni, Augustine Senga, alikiri kutokea mauaji hayo.
Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi saa 8:00 mchana na kwamba familia hiyo ilikuwa inaishi Tabata Mawenzi.

Senga alisema mwanamke huyo alifariki papo hapo baada ya kushambuliwa na kwamba chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika na uchunguzi unaendelea.
Kamanda Senga alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.

Hata hivyo, mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kufanya mauaji hayo, alifanya jaribio la kutaka kujiua lililoshindikana.

Kamanda alipoulizwa kuhusiana na mtuhumiwa huyo kutaka kujiua, alisema kuwa uchunguzi unaendelea.

“Bado ni mapema sana kueleza kila kitu hayo niliyokueleza ni taarifa za awali kwani na huyu mtuhumiwa amekutwa na majeraha shingoni, hivyo masuala ya kazi yake na sababu vinachunguzwa,” alisema Senga.

MKUU WA MKOA AFUNGUA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII

01_0567b.JPG
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Social Media huko Chuoni kwao Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.
02_ccda3.JPG
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (alie simama) akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media), hawapo pichani yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar kwa kushirikiana na Kigamboni Community Centre KCC kutoka Dar es Salam, huko Chuoni kwao Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.
03_68a56.JPG
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimskiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (hayupo pichani).
04_0d2c4.JPG
Mgeni rasmin Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis (wakatikati) waliokaa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media).Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

SIMBA YAPIGWA FAINI YA MILIONI 3/-

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh. milioni tatu kutokana na timu yake kuvaa jezi ambazo hazikuwa na nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.
Mechi hiyo namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom ilichezwa Desemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 13(7) ya Ligi Kuu inayotaka klabu kuheshimu masharti ya udhamini wa Ligi Kuu kwenye mechi zake.
Nayo Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 28(4) kwa kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na Toto Africans iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuvurugika.
Kutokana na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 28(1) inayotawala ligi hiyo